Viongozi wa nchi za pembe ya Afrika wakubaliana kuhusu mkakati wa kupambana na kundi la Al-Shabaab nchini Somalia
2023-02-02 08:27:14| CRI

Viongozi wa nchi nne za pembe ya Afrika wamekubaliana mpango wa utekelezaji wa pamoja wa kupambana na kundi la Al-Shabaab, na kuhamasisha uungaji mkono wa kikanda kwa wakati kwa ajili ya operesheni dhidi ya kundi hilo nchini Somalia.

Marais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia, William Ruto wa Kenya, Ismail Gulelleh wa Djibouti na Waziri Mkuu wa Ethiopia Bw Abiy Ahmed, wamesema watumishi wa usalama waliozatitiwa vizuri, wanakuwa kwenye nafasi nzuri ya kupambana na kundi la Al-Shabaab.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa mjini Mogadishu baada ya mkutano wa siku moja, inasema viongozi hao wameamua kuanzisha utaratibu wa pamoja unaoratibu uwezo wa jumla ili kilikabili na kulishinda kundi la Al Shabaab.

Viongozi hao pia wamekaribisha ombi la Somalia kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la silaha na uungaji mkono mwingine ili kulizatiti jeshi jipya la Somalia na kuimarisha uwezo wa vikosi vyake.