Mjumbe wa China atoa mwito kuungwa mkono zaidi kwa juhudi za Iraq kupambana na ugaidi
2023-02-03 08:33:38| CRI

Naibu mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing ametoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea kuunga mkono juhudi za Iraq za kupambana na ugaidi.

Balozi Dai Bing ameliambia Baraza la Usalama kuwa hali ya sasa ya usalama nchini Iraq bado ni tete, na magaidi waliosalia bado wanafanya mashambulizi yanayosababisha vifo vya raia wasio na hatia.

Balozi Dai amesema Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Iraq (UNAMI) na mashirika mengine ya umoja huo yanapaswa kuhamasisha ukusanyaji wa raslimali na juhudi kwenye maeneo ya kipaumbele yanayohitajika zaidi kwa watu wa Iraq, kufanya kazi kwa mujibu wa mamlaka yao na kuonesha umuhimu kulingana na hadhi yake kama timu ya Umoja wa Mataifa.