CMG kufanya tamasha la sikukuu ya taa la mwaka 2023
2023-02-03 10:38:38| cri

Tarehe 5 Februari, siku ya 15 ya mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo ya China ni sikukuu ya taa, moja ya sikukuu za jadi za China. Tamasha la Taa la 2023 linaloandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG litaonyesha sifa ya kipekee ya sikukuu hiyo ya jadi ya taa zenye mapambo kupitia nyimbo za jadi, opera, michezo ya kuigiza, na aina za sanaa nyingine.

Tangu enzi za zamani, katika sikukuu ya taa, watu huwa wanaisherehekea kwa kutazama taa zenye mapambo, na kwamba taa zenye mapambo zinazoonesha mila mbalimbali za utamaduni wa China zitaonekana kwenye tashama hilo la CMG kwa mwaka huu, ambalo litatangazwa kote duniani.