UNICEF: Mapigano na majanga ya tabianchi yamelazimisha watoto zaidi ya milioni 3.5 kukosa shule nchini Ethiopia
2023-02-03 09:15:08| CRI

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, limesema watoto zaidi ya milioni 3.5 wameshindwa kwenda shule kutokana na athari zinazotokana na mapigano na majanga ya tabianchi nchini Ethiopia.

Kupitia Taarifa ya Robo Mwaka kuhusu Elimu ya Ethiopia iliyotolewa Jumatano, shirika hilo limesema, majanga mbalimbali yanayotokana na vyanzo vya kibinadamu au vya asili yanaendelea kuleta athari kwa Ethiopia, na kuanzia mwaka 2022, watoto zaidi ya milioni 3.5 wamekosa shule kutokana na mapigano na majanga ya tabianchi.

Huko Tigray, taarifa hiyo imeonesha kuwa watoto milioni 1.7 kati ya watoto milioni 2.3 wanaokadiriwa kufikia umri wa kwenda shule wamenyimwa haki ya kupata elimu kwa miaka mitatu ya masomo kutokana na vita na COVID-19, huku uharibifu umeripotiwa kuathiri asilimia 88 ya miundombinu ya shule.