Israel na Sudan kusaini makubaliano ya kurejesha uhusiano wao kwenye hali ya kawaida
2023-02-03 09:00:40| CRI

Waziri wa mambo ya nje ya Israel Bw. Eli Cohen alipokutana na waandishi wa habari baada ya ziara yake nchini Sudan, amesema Israel na Sudan zimekubaliana kusaini makubaliano ya kurejesha uhusiano kati yao kwenye hali ya kawaida baadaye mwaka huu.

Amesema ziara yake imeweka msingi wa kufikia makubaliano ya amani yenye maana ya kihistoria kati ya nchi hizo mbili, ambayo yanatarajiwa kuhimiza utulivu wa kanda na kuchangia usalama wa Israel.

Tangazo moja lililotolewa na Baraza Kuu la Sudan limesema mazungumzo na Israel yanalenga kujenga uhusiano wenye mafanikio kati yao na kuimarisha ushirikiano katika mambo ya usalama na jeshi.

Sudan inatarajiwa kuwa nchi ya nne ya Kiislamu kusaini makubaliano ya kurejesha uhusiano na Israel kwenye hali ya kawaida chini ya Makubaliano ya Abraham.