Waziri wa mambo ya nje wa China afanya mazungumzo na mwenyekiti wa UNGA
2023-02-03 09:02:43| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Qin Gang jana alifanya mazungumzo na mwenyekiti wa kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) Bw. Csaba Korosi hapa Beijing.

Bw. Qin Gang amesema hivi sasa dunia inakabiliwa na changamoto zisizoisha, na pande zote zina matumaini makubwa kuhusu kuendelea kutoa mchango mkubwa kwa Umoja wa Mataifa, katika usimamizi wa dunia.

Amesema Umoja wa Mataifa unapaswa kudumisha amani na usalama, na kulinda haki na usawa, kushikilia manufaa na ushirikishwaji kwa wote, kulinda taratibu za pande nyingi, kuacha makabiliano ya kiitikadi, na kuhimiza kufundishana kati ya staarabu tofauti.

Bw. Korosi amesema China ni mshirika muhimu wa Umoja wa Mataifa na ameishukuru China kwa uungaji mkono wake mkubwa wa miaka mingi kwa Umoja wa Mataifa.