Wahudumu wa usafiri wa umma nchini Kenya wanakumbatia matumizi ya mabasi ya umeme wakati mahitaji ya utaratibu wa usafiri rafiki wa mazingira nchini humo yakiongezeka.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki wa Matatu nchini Kenya (MOA) katika Kaunti ya Nairobi, Christopher Muia amesema, mpaka sasa, mabasi matatu yanayotumia umeme yaliyotengenezwa nchini China yanatoa huduma ya usafiri katika jiji hilo. Ameweka wazi kuwa, karibu asilimia 60 ya idadi ya watu mjini Nairobi wanategemea usafiri wa umma kwa usafiri wao wa kila siku.