Serikali ya Ethiopia kutuma fedha katika mkoa wa Tigray
2023-02-06 10:34:19| CRI

Serikali ya Ethiopia imesema itatuma birrs bilioni 5 (sawa na dola za kimarekani milioni 93) katika mji mkuu wa mkoa wa Tigray, Mekele, wakati ikianza kurejesha huduma za kibenki katika mkoa huo ulioathirika na mgogoro.

Shirika la Utangazaji la Taifa Fana, Jumamosi lilimnukuu Redwan Hussein, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Waziri Mkuu Abiy Ahmed, akisema Benki ya Taifa ya Ethiopia itatuma fedha hizo kuanzia leo Jumatatu.

Ahmed Ijumaa alikutana na viongozi wa Kundi la Ukombozi wa Watu wa Tigray TPLF kwa mara ya kwanza tangu mgogoro huo uliodumu kwa miaka miwili umalizike mwishoni mwa mwaka jana kwa kufikia makubaliano ya amani.