Wizara ya Ulinzi ya China yailalamikia Marekani kwa kushambulia chombo cha anga cha kiraia kisicho na rubani
2023-02-06 10:40:23| CRI

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China Tan Kefei ametoa malalamiko makali dhidi ya kitendo cha Marekani cha kushambulia chombo cha anga cha kiraia kisicho na rubani cha China.

Amesema shambulio hilo la Marekani lilikuwa la kupindukia, na kwamba China inapinga vikali kitendo hicho na ina haki ya kuchukua hatua zinazofaa kukabiliana na hali kama hizo zitakapotokea.

Wakati huohuo mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya Mambo ya Nje ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Bw. Wang Yi alipozungumza kwa njia ya simu na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Antony Blinken siku ya Ijumaa, alitoa wito kwa Marekani kudumisha mawasiliano kati yake na China kwa wakati, kuepusha uamuzi mbaya na kudhibiti tofauti zinazotokea kwa bahati mbaya.

Wang alisema pande hizo mbili zimewasiliana kuhusu jinsi ya kukabiliana na tukio la bahati mbaya kwa njia ya utulivu na ya kitaalamu.

Alisisitiza kuwa kama nchi inayowajibika, China siku zote inafuata sheria za kimataifa na haitakubali uvumi wowote usio na msingi.