China imerejesha usafiri wa makundi ya watalii katika nchi za nje
2023-02-06 19:34:28| cri

Miaka mitatu baada ya janga la UVIKO-19, makundi ya kwanza ya watalii kutoka China yamewasili Jumatatu katika mji mkuu wa Thailand, Bangkok, yakilakiwa kwa maua na makaribisho mazuri kutoka nchi hiyo ya Kusini-Mashariki mwa Asia huku ikiweka tumaini kubwa la kufufuka kwa shughuli muhimu za utalii za nchi hiyo.

Jumatatu asubuhi, maafisa kutoka Idara ya utalii ya Thailand na Ubalozi wa China nchini Thailand walikaribisha makundi mawili ya kwanza ya watalii wapatao 20 kila moja kutoka Guangzhou kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Don Mueang. Watalii hao, ambao wako kwenye mpango wa kutalii kwa siku sita, watazuru Bangkok na kisha kuelekea eneo la kusini kwenye kituo cha mapumziko cha bahari.

Kuwasili kwa makundi haya ya watalii kunakuja wakati ambapo China, moja ya soko kubwa zaidi la utalii duniani kabla ya janga la korona , siku ya Jumatatu wiki hii imeanza tena safari za nje za makundi ya watalii.

Kuanzia Jumatatu, China imerejesha usafiri wa makundi ya watalii katika nchi 20, ikiwemo Thailand, Maldives, Falme za Kiarabu, Russia, na New Zealand.