DRC yalaani shambulizi dhidi ya helikopta ya MONUSCO
2023-02-07 09:36:43| CRI

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imelaani shambulizi dhidi ya helikopta ya Tume ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) kwenye viunga vya mji wa Goma, jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, helikopta hiyo iliwaka moto Jumapili wakati ikisafiri kutoka Beni na kuelekea Goma, ambapo imesababisha mlinda amani mmoja wa Afrika Kusini kuuawa na mwengine kujeruhiwa vibaya. Na helikopta hiyo ilifanikiwa kutua Goma.

Kwenye taarifa iliyotolewa Jumatatu na msemaji wa serikali Patrick Muyaya, imesisitiza kuwa shambulizi hilo lilitokea kwenye eneo linalokaliwa na waasi wa kundi la M23, wakiungwa mkono na Jeshi la Rwanda (RDF), saa 24 baada ya kutolewa amri ya kuweka silaha chini huko Bujumbura, nchini Burundi, iliyotolewa na wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Hadi sasa hakuna kundi lililotangaza kuhusika na shambulizi hilo.