Serikali ya mpito ya Mali imesema kuwa mkuu wa kitengo cha haki za binadamu cha kikosi cha ulinzi wa amani cha Umoja wa Mataifa nchini humo Guillaume Ngefa-Atondoko Andali amepewa saa 48 kuondoka nchini humo na kutangazwa kuwa mtu asiyekubaliwa nchini humo.
Katika taarifa yake, serikali hiyo imesema uamuzi wa kumfukuza mkuu huyo unahusiana na tuhuma za upendeleo wake kwa mashahidi wa mashirika ya kijamii katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Mali kilichofanyika Januari 27.