Xi atoa rambirambi kwa rais wa Uturuki na Syria kufuatia tetemeko la ardhi
2023-02-07 09:33:22| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za rambirambi kwa wenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Syria Bashar al-Assad kufuatia matetemeko makubwa ya ardhi yaliyotokea katika nchi hizo mbili.

Xi ameeleza kushtushwa kwake na habari ya matetemeko makubwa ya ardhi yaliyosababisha vifo na majeruhi wengi pamoja na hasara kubwa ya mali nchini Uturuki na Syria. Kwa niaba ya serikali ya China na watu wake, Xi alitoa salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa pamoja na majeruhi. Amesema anaamini kuwa chini ya uongozi wa rais Erdogan na rais Bashar, serikali za nchi hizo mbili na wananchi wake watashinda maafa na kujenga upya makazi yao haraka.

Wakati huohuo, Chama cha Msalaba Mwekundu cha China kimeamua kutoa fedha taslimu dola laki mbili za kimarekani kwa vyama vya hilali nyekundu vya Uturuki na Syria mtawalia kama msaada wa dharura wa kibinadamu.