Kituo cha huduma za uchumi na biashara ya kidijitali kati ya China na Afrika cha Hunan chaanzishwa Changsha
2023-02-07 21:18:16| cri

Kituo cha huduma za kidijitali za uchumi na biashara kati ya China na Afrika cha mkoa wa Hunan kimezinduliwa jana Jumatatu mjini Changsha. Kituo hicho kinatarajiwa kuunga mkono ujenzi wa uwezo wa kidijitali na TEHAMA kwenye ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika, na pia kitazisaidia baadhi ya nchi za Afrika kujenga mfumo wa malipo ulio kamili na wenye ufanisi zaidi.

Kituo hicho kimeanzishwa kwa pamoja na kampuni ya Unicom ya Hunan na Shirika la kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika la mkoa wa Hunan, na kinalenga kutoa huduma za dijitali na TEHAMA kwa kampuni za China barani Afrika, ili kuchangia maendeleo yenye ubora ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya pande hizo mbili.