Wamarekani wenye asili ya Afrika waliougua UVIKO-19 kwa muda mrefu wateseka kupata huduma za afya
2023-02-08 10:09:37| CRI

Katika kipindi chote cha janga la UVIKO-19, Wamarekani wenye asili ya Afrika ndio watu walioathirika zaidi, waliolazwa hospitalini zaidi na waliokufa zaidi wakilinganishwa na watu wa jamii nyingine, na sasa madaktari na watetezi wanaonya kuwa watu hawa wanakabiliwa na kizuizi kingine ambacho ni upatikanaji wa huduma za afya kwa wale wenye dalili za muda mrefu za virusi vya corona.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Utafiti wa Pulse wa Bodi ya Sensa ya Nyumba wa Marekani, uliofanyika Januari 4 na 16, asilimia 28.7 ya Wamarekani wenye asili ya Afrika waliohojiwa wanasema sasa hivi wanazo ama walikuwa nazo dalili za virusi vya Corona kwa muda mrefu.

Kuugua kwa muda mrefu virusi vya Corona ni pale baada ya mgonjwa aliyeambukizwa UVIKO-19 kuendelea kuonesha dalili za ugonjwa kwa zaidi ya wiki nne baada ya kupona. Kwa baadhi ya watu dalili hizi huendelea kwa miezi kadhaa au hata miaka.