Xi asisitiza kufahamu na kuendeleza maendeleo ya kisasa ya China
2023-02-08 10:15:12| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza umuhimu wa kuelewa kwa usahihi na kuboresha kwa nguvu maendeleo ya kisasa ya China.

Kauli hiyo ameisisitiza kwenye ufunguzi wa semina ya chuo cha kamati kuu ya CPC, ambapo amesema kutimiza ustawishaji mkubwa wa taifa la China yamekuwa matarajio ya pamoja ya watu wa China tangu kuanza kwa zama za sasa, na kuongeza kuwa kazi ya kihistoria ya kuchunguza njia ya China ya kisasa imeanguka kwenye mabega ya CPC.

Xi pia amesisitiza kuwa tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China ufanyike mwaka 2012, Chama kimepata maendeleo mapya kulingana na uchunguzi wa awali, na kuendelea kupata uvumbuzi na mafanikio katika nadharia na vitendo, pamoja na kuendeleza kwa mafanikio na kupanua maendeleo ya kisasa ya China.

Rais Xi amebainisha kuwa mafanikio na mabadiliko ya kihistoria, hasa kuondoa umaskini uliokithiri na kukamilika kwa ujenzi wa jamii yenye ustawi wa wastani katika nyanja zote, yamepelekea kuwa na taasisi imara zaidi, misingi imara ya nyenzo, na chanzo cha msukumo wa kuchukua hatua kubwa zaidi kwa ajili ya maendeleo ya kisasa ya China.