Guterres aonya upotevu wa amani
2023-02-08 19:28:26| cri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya juu ya uwezekano wa vita kati ya Russia na Ukraine kuwa inaweza kuenea zaidi na kuchochea upotevu wa amani duniani.

Akizungumza wakati akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Guterres amesema vita hiyo imesababisha mateso makubwa kwa watu wa Ukraine, ikiambatana na athari kubwa kwa dunia nzima.

Guterres pia amekemea vitisho vya kutumia silaha za maangamizi, akisema kile kinachozungumzwa na Russia kuhusu matumizi ya nyuklia ya kimkakati hakina tija kimantiki.