Msemaji wa kundi la waasi la TPLF Bw. Getachew Reda amesema, licha ya kuondoka kwa vikosi vya Eritrea kutoka Tigray, bado kuna vikundi vidogo vya wanajeshi wa nchi hiyo ambao wamebaki kwenye eneo hilo.
Bw. Reda amesema hayo alipokutana na wanahabari baada ya mkutano wa kwanza kati ya maofisa wa TPLF na Waziri Mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed. Ameongeza kuwa walikubaliana na waziri mkuu huyo kwenye mkutano uliofanyika wiki iliyopita, kwamba vikosi vya serikali vinapaswa kupelekwa kwenye maeneo yanayopakana na Eritrea, ili kuhakikisha usalama kama ilivyokubaliwa kwenye makubaliano ya amani ya Pretoria.