Umoja wa Mataifa umesema, watu waliouawa katika shambulizi lililofanywa na waasi wa kundi la M23 mashariki kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mwezi Novemba mwaka jana ni 171, na si 131 iliyotajwa awali.
Katika waraka unaoeleza uhalifu uliofanyika nchini DRC mwaka jana, Ofisi ya Pamoja ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema, waasi wa M23 waliwaua raia 171 katika eneo la makazi la Kishishe na Bambo, mashariki mwa mkoa wa Kivu Kaskazini nchini DRC.
Uchunguzi wa awali uliofanywa na Umoja wa Mataifa uligundua kuwa raia 131 waliuawa katika shambulizi hilo.