Serikali ya Ethiopia imesema reli iliyojengwa na China ya Ethiopia-Djibout imetoa mchango mkubwa katika sekta ya uagizaji na usafirishaji bidhaa ya Ethiopia.
Kauli hiyo imetolewa baada ya maafisa waandamizi wa Ethiopia pamoja na Abdi Zenebe, afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya pamoja ya reli ya Ethiopia-Djibout, kutembelea reli hiyo. Kwenye taarifa yake Wizara ya Uchukuzi na Ugavi ya Ethiopia imesema kuwa reli hiyo imeongeza sana aina na kiasi cha usafirishaji wa mizigo, na mwisho kuongeza mchango wake katika sekta ya uagizaji na usafirishaji bidhaa, kutoka asilimia 11 hadi asilimia 15 ya sasa ndani ya mwaka mmoja.
Naye Waziri wa wizara hiyo Denge Boru amebainisha kuwa reli hiyo zaidi imechangia kupunguza muda wa ugavi na gharama na pia kutoa huduma zenye ufanisi kwa wasafirishaji wanaosambaza bidhaa katika soko la nje.