Barabara ya mwendo kasi ya Nairobi yenye urefu wa kilomita 27.1, iliyojengwa na kampuni ya China kwa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi, Jumanne iliwatambua madereva milioni kumi ambao wameitumia barabra hiyo tangu ilipozinduliwa rasmi Julai 2022.
Maofisa wakuu, watendaji wakuu na madereva wa kawaida wa magari walihudhuria hafla hiyo kuadhimisha kufikia watumiaji milioni kumi kwenye barabara hiyo ya kisasa ambayo imerahisisha usafiri kutoka kusini mwa mji wa Nairobi ulipo uwanja wa ndege, hadi wilaya ya juu ya Westlands.
Katibu Mkuu anayeshughulikia mambo ya barabara Bw. Joseph Mbugua, ameitaja barabara ya mwendokasi ya Nairobi Expressway mradi wa miundombinu ambao umeimarisha usafirishwaji wa watu na mizigo, na kuifanya Kenya kuwa kitovu cha kibiashara na ugavi.