China yapiga hatua kuharakisha mageuzi ya kilimo nchini Uganda
2023-02-09 10:38:52| CRI


Karibu tena msikilizaji katika kipindi hiki cha Daraja kinachokujia kila jumapili kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

katika kipindi cha leo tutakuwa na ripoti inayohusu jinsi China inavyowasaidia wakulima nchini Uganda kuongeza tija kutokana na kilimo, na pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi, ambayo yatazungumzia Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Egerton nchini Kenya inavyotoa fursa kwa mamia ya wanafunzi wa chuo hicho kusoma lugha ya Kichina, lugha ambayo inaendelea kupata umaarufu katika nchi mbalimbali duniani.