Watu 24 wameuawa na wengine 53 kujeruhiwa katika siku ya pili ya mapigano makali katika eneo linalotaka kujitenga na Somalia, Somaliland, baada ya viongozi wa eneo hilo kutangaza nia ya kujiunga tena na serikali kuu ya Somalia.
Somaliland ilijitenga na Somalia mwaka 1991 lakini haijatambuliwa kimataifa kuwa ni taifa huru, na wakati huohuo, mkoa huo unakabiliwa na upinzani kutoka kwa baadhi ya viongozi wa makabila katika eneo la mashariki ambao wanataka kuwa chini ya serikali ya Somalia.
Mkoa huo umesema, wapiganaji kutoka mkoa wa jirani wa Puntland walikuwa wakipigana bega kwa bega na wanamgambo wa eneo hilo katika mji wa Las Anod, madai ambayo mkoa wa Puntland umeyakana.