Rais wa China ajibu barua ya madaktari wanaotoa msaada barani Afrika
2023-02-10 14:29:49| cri

Rais Xi Jinping wa China amejibu barua ya madaktari wa China wanaotoa msaada nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, akiwahimiza kutoa mchango zaidi kwa ajili ya ujenzi wa jumuiya ya afya ya binadamu wote yenye hatma ya pamoja.

Kwenye barua yake rais Xi amesema wao ni madaktari wanaookoa maisha, pia ni mabalozi wanaoeneza urafiki. Ameongeza kuwa huu ni mwaka wa 60 tangu China ianze kutuma madaktari kwa nchi nyingine, na ametoa salamu kwa wachina wanaotoa na waliotoa msaada wa matibabu katika nchi za nje. 

Mwaka 1963 China ilituma kikundi cha kwanza cha madaktari nchini Algeria. Katika miaka 60 iliyopita, China imetuma madaktari 30,000 kwa nchi 76 za Afrika, Asia, Amerika, Ulaya na Oceania, na kuwatibu wagonjwa milioni 290.