Maafisa wa Somalia na Umoja wa Afrika wameeleza kuridhishwa na operesheni inayoendelea dhidi ya kundi la al-Shabaab na kupongeza hatua iliyopigwa katika kurejesha amani na usalama nchini Somalia.
Waziri wa Habari, Utamaduni na Utalii wa Somalia Daud Aweis na mwakilishi maalumu wa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ambaye pia ni Mkuu wa Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) Mohammed El-Amine Souef, wamesema magaidi kadhaa sasa wamejisalimisha serikalini huko HirShabelle, Galmudug na Kusini Magharibi.
Kwenye taarifa yao ya pamoja iliyotolewa Mogadishu, Aweis amesema magaidi waliojisalimisha watapitia mchakato wa kuwaponya kabla ya kuruhusiwa kujiunga na jamii.