Wanaanga wa China wa chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-15 wafanikiwa kukamilisha jukumu lao la kwanza la nje
2023-02-10 09:54:18| CRI

Shirika la Anga ya Juu la China limesema, Wanaanga wa China wa chombo cha Shenzhou-15 ambao wako kwenye kituo cha anga ya juu cha China cha Tiangong kinachozunguka wamekamilisha matembezi yao ya kwanza nje ya chombo kwenye anga ya juu Saa 6:16 Asubuhi (Saa za Beijing) siku ya Ijumaa.

Wanaanga hao Fei Junlong na Zhang Lu, pamoja na Deng Qingming ambaye alifanya kazi ndani ya kituo cha anga za juu ili kusaidia wanaanga wenzake, walishirikiana kukamilisha kazi zote zilizopangwa. Fei na Zhang wamerejea salama kwenye moduli ya maabara ya Wentian.

Wakati wakifanya shughuli za ziada (EVAs) zilizochukua takriban saa saba, walikamilisha kazi kadhaa, ikiwa ni pamoja na usakinishaji wa pampu za upanuzi nje ya moduli ya maabara ya Mengtian.

Hizi zilikuwa ni shughuli za ziada za mara ya kwanza kufanywa baada ya kukamilika kwa kituo cha anga ya juu cha China. Wanaanga hao wa Shenzhou-15, kama ilivyopangwa, watafanya matembezi kadhaa nje ya chombo kwenye anga ya juu katika siku zijazo, limesema shirika hilo.