Raia wanane wauawa katika mapigano na askari wa UM mashariki mwa DRC
2023-02-10 22:06:33| cri

Raia wanane wameuawa na wengine 28 kujeruhiwa baada ya waandamanaji katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuzuia msafara wa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo (MONUSCO) jumanne jioni katika eneo la Munigi, karibu na Goma.

Taarifa iliyotolewa na Tume hiyo imesema, raia hao waliuawa wakati wa shambulizi kali dhidi ya msafara wa MONUSCO ambao ulikuwa ukielekea Goma ukiwa pamoja na askari wa DRC. Askari hao walishambuliwa na waandamanaji ambao walifunga barabara kwa kutumia mawe na hivyo kulazimisha msafara huo kusimama.

Taarifa hiyo pia imesema, waandamanaji hao walichoma moto magari manne yaliyokuwa kwenye msafara huo na kuiba mali zilizokuwemo katika magari hayo.