Burundi yapongeza mchango wa wataalamu wa China katika sekta ya kilimo nchini humo
2023-02-13 08:38:53| CRI

Katibu wa Waziri wa Mazingira, Kilimo na Mifugo nchini Burundi, Emmanuel Ndorimana amesema, nchi hiyo imeridhika kwa kiwango kikubwa na mafanikio ya timu ya tano ya wataalamu wa kilimo kutoka China waliomaliza jukumu lao nchini humo.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wataalamu hao iliyofanyika kwenye Ubalozi wa China nchini Burundi, Bw. Ndorimana amesema hiyo ni fursa kubwa kwa serikali ya Burundi kutoa shukrani zake kutokana na mafanikio yaliyopatikana chini ya timu hiyo ya wataalamu wa kilimo kutoka China.

Kwa upande wake, Balozi wa China nchini Burundi, Zhao Jiangping amesema, ushirikiano wa kilimo kati ya nchi hizo mbili ulioanzia mwaka 1984 ni sekta muhimu na iliyotangulia  katika ushirikiano wa kimkakati kati ya Burundi na China ulioleta manufaa makubwa kwa pande hizo mbili.