Matetemeko ya ardhi yawaua watu zaidi ya 30,000 katika nchi za Uturuki na Syria
2023-02-13 08:38:14| cri


 

Idadi ya watu waliofariki kutokana na matetemeko ya ardhi yaliyotokea tarehe 6 nchini Uturuki na Syria imeongezeka na kufikia 29,605 na 1,414.

Kutokana na takwimu za kiserikali, idadi ya majeruhi nchini Uturuki na Syria imefikia 80,000 na 2,349.

Waziri wa sheria wa Uturuki Bw. Bekir Bozdag amesema, Uturuki imetoa amri ya kuwakamata watuhumiwa 134 waliohusika na makosa ya ujenzi wa majengo yaliyoanguka kwenye matetemeko ya ardhi, na watatu kati yao tayari wamekamatwa.