Watalii 40 kutoka China wamewasili nchini Kenya kwa ajili ya kufanya utalii, ikiwa ni kikundi cha kwanza cha watalii kutoka China kufika nchini Kenya baada ya China kurejesha safari za nje kwa makundi ya watalii.
Balozi mdogo wa utamaduni wa China nchini Kenya Tang Jianjun amesema, watalii wa China wataleta imani kwa sekta zinazohusika za utalii za Kenya, na kuingiza msukumo kwa maendeleo ya jamii na uchumi nchini humo.
Mwaka huu ni miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Kenya. Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Kenya inaweka mkazo mkubwa katika soko la utalii la China, na kuimarisha utangazaji wa utalii nchini China.