Kampeni ya ukusanyaji taka Tanzania yalenga kukuza utalii endelevu
2023-02-13 08:37:52| cri

Kampeni ya  Usafi wa Miji Tanzania inayojihusisha kukusanya taka katika maeneo yenye vivutio vya utalii wa nchi hiyo katika jiji la Arusha na Dar es Salaam, manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro na Kisiwa cha Zanzibar, imeanzishwa nchini Tanzania.

Akizungumza katika hafla ya kuanzishwa kwa kampeni hiyo, , Shakira Athuman mwenye miaka 17, aliyemaliza kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Open Joy iliyopo Mbweni jijini Dar es Salaam Desemba 2022, amesema, miji ikiwa katika hali ya usafi hakutakuwa na magonjwa ya kuambukiza, na pia watalii kutoka nchi mbalimbali watavutiwa kutembelea vivutio vya utalii nchini kwetu .

 Usafi wa Miji Tanzania ni kampeni iliyoanzishwa mapema mwaka huu kwa lengo la kufanya usimamizi wa taka katika miji ya Arusha na Dar es Salaam, manispaa ya Moshi na Kisiwa cha Zanzibar kwa lengo la kukuza utalii endelevu.