Shirika la Ndege la Ethiopia limetangaza kuwa limeongeza miji ya Xiamen na Shenzhen kusini mwa China katika safari zake za ndege za mizigo.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa ijumaa iliyopita, Shirika hilo limesema limeanza safari mbili kwa wiki za ndege za mizigo inayounganisha mji wa Xiamen na mji wa Sao Paulo wa nchini Brazil, na mji mkuu wa Chile, Santiago, kupitia mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.
Taarifa hiyo pia imesema, kuanzia ijumaa wiki hii, Shirika la Ndege la Ethiopia linapanga kuanzisha safari za mara mbili kwa wiki kati ya mji wa Shenzhen na mji wa Liege nchini Ubelgiji.
Tayari Shirika la Ndege la Ethiopia linafanya safari za ndege za mizigo katika miji ya Guangzhou, Shanghai, Zhengzhou, Changsha na Wuhan nchini China.