Uturuki yawakamata wakandarasi, wahandisi wanaohusika na majengo mabovu katika eneo la tetemeko
2023-02-13 10:29:14| CRI

Waziri wa Sheria wa Uturuki Bw. Bozda alisema jioni ya tarehe 12 kuwa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Uturuki ilitoa hati 134 za kuwakamata wakandarasi na wahandisi waliohusika moja kwa moja na majengo mabovu katika eneo la tetemeko la ardhi.

Bw. Bozda amesema ofisi ya Mwendesha Mashtaka ilianzisha“Ofisi ya Uchunguzi wa Uhalifu wa Tetemeko la Ardhi”katika mikoa 10 iliyoathiriwa na tetemeko hilo ili kuchunguza kwa pande zote kuanguka kwa idadi kubwa ya majengo wakati wa tetemeko hilo.