Rwanda yasisitiza ahadi yake ya kuunga mkono wanasayansi wanawake
2023-02-13 08:39:41| CRI

Rwanda imethibitisha tena ahadi yake ya kuwaunga mkono wasichana na wanawake  katika sayansi na kuongeza upatikanaji wa fursa za elimu na mafunzo katika sekta ya sayansi na teknolojia.

Hayo yamesemwa katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi inayofanyika Februari 11 kila mwaka.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Waziri wa Jinsia na Familia wa nchi hiyo  Jeannette Bayisenge amesema, sayansi ni chombo chenye nguvu kinachosaidia kuelewa na kuboresha mazingira, na ni muhimu kwa wanawake na wasichana kuwa na fursa ya kushiriki katika sekta hiyo na kutoa mchango wao.

Amewataka wazazi wa watoto kuondokana na upendeleo wa kijinsia ambao mara nyingi unawakataza wanawake na wasichana kutotafuta ajira zinazohusiana na sayansi, teknolojia, uhandisi na hesabu.