Ndege ya pili ya msaada kutoka China yawasili Syria
2023-02-14 08:33:25| cri

Shehena ya pili ya misaada kutoka Chama cha Msalaba Mwekundu cha China (RCSC) imewasili Syria jana Jumatatu ikiwa na vifaa vya dharura kwa watu walioathiriwa na matetemeko ya ardhi nchini humo.

Balozi wa China nchini Syria Bw. Shi Hongwei amesema, msaada huo ni pamoja na mavazi ya majira ya baridi, vifaa, dawa, na vitu vingine muhimu vinavyohitajika, na kuongeza kuwa msaada zaidi utapelekwa katika siku zijazo.

Balozi Shi pia amezitaka Marekani na nchi za Magharibi kuondoa vikwazo dhidi ya Syria ili kurahisisha misaada kupelekwa kwa watu wanaohitaji nchini humo.