Timu ya uokoaji ya China yawaokoa watu 6 nchini Uturuki
2023-02-14 08:35:06| cri



Timu ya uokoaji ya China imewaokoa watu 6 huko mji wa Antakya, uliokumbwa na matetemeko la ardhi nchini Uturuki. 

Jumapili alasiri, baada ya juhudi za saa 4, timu ya uokoaji ya China ikishirikiana na ya Uturuki ilimwokoa mwanamume mwenye umri wa miaka 50, na mpaka sasa, timu ya uokoaji ya China imetuma vikundi 13 vya waokoaji 206, kuwaokoa watu 6, na timu ya uokoaji kutoka Hong Kong, China iliwaokoa watu watatu.