Guterres aikaribisha serikali ya Syria iongeze forodha za kupokea msaada kutoka nje kwa ajili ya tetemeko la ardhi
2023-02-14 18:45:25| cri

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres tarehe 13 mwezi Februari alitoa taarifa kupitia msemaji wake akisema anaikaribisha serikali ya Syria iongeze forodha za kupokea msaada kutoka nje kwa ajili ya tetemeko la ardhi.

Guterres amemshauri rais Bashar al-Assad wa Syria kufungua forodha mbili kutoka Uturuki hadi kaskazini magharibi mwa Syria, ili kutekeleza uamuzi wa kupeleka msaada wa kibinadamu ambao una muda wa miezi mitatu sasa.

Guterres ameongeza kuwa ni jambo muhimu kwa sasa kuwapatia mamilioni ya waathirika wa tetemeko la ardhi vitu vya msaada. Kufungua forodha hizo, kuhimiza kuidhinishwa kwa misaada ya kibinadamu, kuharakisha utoaji wa viza na kulegeza udhibiti wa safari kati ya vituo vya mawasiliano, kutawezesha kuingia kwa misaada mingi zaidi na kwa haraka zaidi.