Watu 20 wauawa katika mashambulizi nchini Burkina Faso
2023-02-14 08:41:18| CRI

Vyanzo vya Usalama vya Burkina Faso vimesema, takriban watu 20 wakiwemo askari mgambo, wameuawa katika mashambulizi mawili yaliyofanywa na watu wenye silaha kwenye maeneo ya kaskazini magharibi na mashariki mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, kundi la kigaidi lenye silaha lilivamia kijiji cha Yargatenga, jimbo la Koulpelogo, eneo la Centre-Est usiku wa Jumapili, na kuua watu kumi, ikiwa ni pamoja na watu wawili wa kujitolea wa ulinzi wa taifa (VDP).

Siku ya Alhamisi wanachama zaidi ya saba wa VDP waliuawa katika mapigano na kundi la kigaidi lenye silaha huko Dembo, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.