Waziri wa Nishati wa Tanzania Bw. January Makamba amesema hadi kufikia mwaka 2025 Tanzania itakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 5,000 za umeme kulingana na miradi inayotekelezwa sasa.
Akiongea Ikulu mjini Dar es salaam kwenye hafla ya utiaji saini wa mikataba ya uimarishaji wa gridi ya taifa, Bw. Makamba amesema kwa sasa Tanzania inazalisha megawati 1,700 ambazo hazitoshi kwa mahitaji ya nchini, lakini hadi kufikia mwaka 2025 uzalishaji wa umeme nchini Tanzania utakuwa mara tatu zaidi ya uzalishaji wa umeme uliopo sasa.
Pia amesema kwa sasa Tanzania ina njia kuu za kusafirisha umeme zenye urefu wa kilometa 6,000 lakini mahitaji ni kilometa 12,000.