OPEC yakadiria mahitaji ya mafuta duniani yataongezeka mwaka 2023
2023-02-15 21:21:17| cri

Ripoti ya mwezi wa Februari iliyotolewa na Shirika la nchi zinazozalisha mafuta duniani (OPEC) inakadiria kuwa kasi ya ongezeko la mahitaji ya mafuta duniani kwa mwaka 2023 itakuwa mapipa milioni 2.3 kwa siku, na makadirio ya hapo zamani yalikuwa ni mapipa milioni 2.22 kwa siku. Wakati huohuo, OPEC inaongeza makadirio kuhusu ongezeko la uchumi wa dunia katika mwaka 2023 hadi kufikia asilimia 2.6 kutoka asilimia 2.5 ya awali, na kuongeza makadirio kuhusu ongezeko la uchumi wa nchi zinazotumia Euro kwa mwaka 2023 hadi asilimia 0.8 kutoka asilimia 0.4.