Kampuni za China zachangia fedha kuunga mkono mradi wa chakula katika shule nchini Kenya
2023-02-15 08:31:45| CRI

Shirikisho la kampuni za China nchini Kenya zimechangia fedha kuunga mkono mradi wa chakula katika Shule ya Mcedo Beijing iliyoko eneo la makazi duni la Mathare mjini Nairobi, Kenya.

Hafla hiyo iliyoambatana na kukabidhi madarasa yaliyokarabatiwa, ilihudhuriwa na mabalozi, maofisa wa ngazi ya juu kutoka Shirikisho la Uchumi na Biashara la Kenya na China, waalimu, wanafunzi pamoja na wazazi.

Ofisa wa ngazi ya juu wa Ubalozi wa China nchini Kenya Zhang Yijun amesema, mchango huo wa upatikanaji wa mlo wa asubuhi na mchana kwa wanafunzi utawashawishi kusoma kwa bidii na kutimiza ndoto zao.