Mkutano wa kilele wa BRICS kujadili urekebishaji wa mpango wa kimataifa wa kisiasa na kiuchumi
2023-02-15 08:31:48| cri

Naibu Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini Bw. Alvin Botes amesema, mkutano wa kilele wa BRICS utakaoandaliwa na nchi hiyo mwaka huu utajadili jinsi ya kurekebisha mpango wa kimataifa wa kisiasa, kiuchumi na kifedha.

Amesema uenyekiti wa Afrika Kusini wa BRICS wa mwaka huu utakuwa na mada: BRICS na Afrika: Ushirikiano wa Pamoja na Ukuaji wa Kasi wa Kuheshimiana, Maendeleo Endelevu na Ushirikiano wa Pande Zote.

Botes amesema, ikiwa nchi pekee ya Afrika katika kundi la BRICS, Afrika Kusini imeendelea kuliweka bara la Afrika na Dunia ya Kusini kwenye ajenda katika maeneo hayo.