China kuendelea kuonesha umuhimu wa kiujenzi katika utatuzi wa suala la madeni ya Zambia
2023-02-15 08:35:49| cri


 

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin jana alipozungumzia suala la madeni ya Zambia amesema, pande husika za suala hilo zinatakiwa kuelewana, kuaminiana, na kufanya juhudi kwa pamoja ili kutafuta mpango mwafaka wa utatuzi.

Amesema China itaendelea kufanya mawasiliano na majadiliano ya kirafiki pamoja na Zambia na pande nyingine husika, na kuonesha umuhimu wa kiujenzi kwa ajili ya utatuzi wa suala hilo.