UM wazindua miradi midogo ya umeme wa jua kuongeza upatikanaji wa umeme nchini Somalia
2023-02-15 08:30:55| CRI

Shirika la Mpango wa Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP) na serikali ya Somalia zimezindua mradi wa mitambo midogo ya umeme wa jua ili kuongeza upatikanaji wa umeme nchini humo.

Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini Somalia Jocelyn Mason amesema katika taarifa ya pamoja iliyotolewa jumatatu wiki hii mjini Mogadishu kuwa, asilimia 65 ya watu hawana umeme nchini Somalia. Amesema mradi wa Mitambo Midogo ya Umeme Afrika (AMP) italeta fursa mpya za maendeleo katika maeneo ya vijijini huku ikichangia kuiweka nchi hiyo katika njia ya maendeleo endelevu.

Mradi huo unaofadhiliwa na Taasisi ya Mazingira ya Dunia (GEF) na Mradi wa Mitambo Midogo ya Umeme Afrika, ni mradi wa upatikanaji umeme wa kikanda unaoongozwa na UNDP kwa kushirikiana na Taasisi ya Milima ya Rocky ya Colorado ambayo inasimamia miradi ya mwelekeo wa nishati duniani, na Benki ya Maendeleo ya Afrika.