Msemaji mkuu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric, jana amesema, Tume ya Ulinzi wa Amani ya Umoja huo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imeripoti hali ya wasiwasi wakati wakisaidia kuandaa uchaguzi wa kwanza kufanyika nchini humo tangu mwaka 1988.
Dujarric amesema, Tume hiyo imeripoti matukio kadhaa ya milipuko katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo katika wiki iliyopita.
Bw. Dujarric amesema, jumanne wiki hii, Tume hiyo ilisaini mpango wa usalama pamoja na serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambayo yatawezesha kufanyika kwa uchaguzi wa amani na kushirikisha pande zote nchini humo