China yaitaka Marekani kuacha mashaka ya kupita kiasi kuhusu China
2023-02-16 20:18:04| cri

Hivi karibuni puto moja la uchunguzi wa hali ya hewa la China ambalo lilifika Marekani kwa bahati mbaya limefuatiliwa sana na Wamarekani. Kutoka kugundua puto hilo tarehe Mosi hadi kuiliangusha kwa makombora tarehe 4 mwezi huu, baadhi ya wanasiasa wa Marekani wametumia fursa hiyo kuchochea wazo la “Matishio ya China”. Baraza la juu la bunge la Marekani lilipitisha maazimio mawili ya kulaani puto la China kukiuka mamlaka ya Marekani.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wang Wenbin alisema maazimisho hayo ya Marekani haina msingi wowote, na ni vitendo vya kisiasa vyenye malengo mabaya, China inapinga kithabiti maazimisho hayo.