Msaada wa serikali ya China kwa Syria wawasili Damascus
2023-02-16 22:21:39| cri

Ndege iliyobeba msaada wa serikali ya China kuelekea Syria kwa ajili ya misaada ya tetemeko la ardhi imewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Damascus. Shehena ya msaada huo inajumuisha takriban vifurushi vya huduma ya kwanza elfu 30, nguo za pamba elfu 10, mahema 300, mablanketi elfu 20, vipande elfu 70 vya taulo za dharura, na vifaa vya matibabu ya dharura kama vile mashine za kupumulia, mashine za ganzi, mashine za oksijeni na taa za upasuaji zisizo za kivuli na kadhalika.