China yatoa msaada wa chakula na lishe kwa Togo
2023-02-16 08:34:08| CRI

Uzinduzi wa mradi wa utoaji wa msaada wa chakula na lishe kwa Togo ambao ulitekelezwa kwa ushirikiano na serikali ya China na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) umefanyika Lome, mji mkuu wa Togo.

Waziri wa Jamii, Maendeleo ya Wanawake, na Kufuta Ujinga wa Togo Adjovi Lolonyo Apédoh-Anakoma amesema, anaamini kuwa kutokana na misaada ya serikali ya China na jumuiya ya kimataifa, serikali ya Togo itaweza kuboresha suala la usalama wa chakula, na kuinua kiwango cha maisha ya wananchi.

Balozi wa China nchini Togo Chao Weidong amesema, lengo la China kushirikiana na WFP kuzindua mradi huo ni kuunga mkono juhudi za serikali ya Togo kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na kuharakisha utekelezaji wa mpango wa dharura wa kuboresha maisha ya wakazi kwenye sehemu ya malisho.

Mwakilishi wa WFP nchini Togo Aboubacar Koisha amesisitiza kuwa, Shirika hilo linapenda kuchangia zaidi katika suala la usalama wa chakula nchini Togo.