Mkutano wa AU watoa wito kuharakisha ushikamano wa Afrika
2023-02-16 08:35:45| cri

Mkutano wa 42 wa siku mbili wa baraza la utekelezaji la Umoja wa Afrika (AU) ulifunguliwa jana kwenye makao makuu ya Umoja huo mjini Addis Ababa, Ethiopia, na kuzitaka nchi za Afrika kuongeza juhudi za kusukuma mbele mshikamano wa Afrika na kushirikiana kutimiza malengo ya maendeleo ya bara hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat amesema, kwa mujibu wa utekelezaji wa mpango wa kwanza wa miaka kumi (2014-2023) wa "Ajenda ya mwaka 2063" ya Umoja wa Afrika, bara hilo limepata mafanikio makubwa katika maendeleo endelevu na ukuaji wa uchumi. Ametoa wito wa kukuza uchumi wa viwanda na kuharakishwa ujenzi wa eneo huria ya biashara barani humo.