Mamlaka ya Udhibiti wa Ukame nchini Kenya (NDMA) imesema, watu milioni 6 katika kaunti za nchini humo zinakabiliwa na uhaba wa chakula kufuatia kipindi kirefu cha ukame nchini humo.
Tathmini iliyofanyika kuanzia Januari 11 hadi Februari 10 imesema, ukame wa muda mrefu umeongeza mgogoro wa njaa katika kaunti za jangwani nchini Kenya, kutishia utulivu na masikilizano. Mamlaka hiyo imeonya kuwa, kutokana na misimu mitano mfululizo ya uhaba wa mvua, athari za janga la COVID-19, gharama kubwa za kilimo na uvamizi wa viwavi jeshi, hali nchini Kenya inaweza kuendelea hadi msimu wa mvua wa mwezi Machi hadi Mei utakapoanza.